
Wimbi kali la joto lisilo la kawaida limeikumba Tunisia, na kusababisha viwango vya joto kupanda hadi karibu nyuzi joto 50 Selsiasi na kuvunja rekodi za kihistoria katika maeneo kadhaa nchini humo.
Wahunzi na waokaji wa mikate ya kienyeji nchini Tunisia kwao imekuwa pigo maradufu kwani joto kali limezidishwa na moto wa majiko pamoja na zana zao za kazi.
Watu wamekuwa wakijipoza kwa kunywa maji na kutoka nje ya nyumba.
Vyombo vya habari nchini Tunisia vimeinuku Mamlaka ya Hali ya Hewa ya nchi hiyo na kuripoti kuwa wimbi la joto juzi Ijumaa lilifikia kilele chake baada ya kusababisha viwango vya juu vya joto liliso la kawaida nchini humo.
Katika mkoa wa Kairouan hali ya hewa ilisajiliwa kuwa nyuzi joto 49.7 Selsiasi, kiwango kilichovunja rekodi yake ya awali ya nyuzi joto 49.2.
Katika jimbo la kaskazini-mashariki la Zaghouan, joto liliripotiwa kufika nyuzi joto 48.6, na kuvunja rekodi ya awali ya nyuzi joto 48.
Baadhi ya watu pia walienda kuogelea huku wengine wakikimbilia maeneo yenye miti na majani ili kupata nafuu kutokana na joto kali.