KLABU ya Ceasiaa Queens imepanga kufanya maboresho makubwa ya kikosi kwenye dirisha hili la usajili baada ya kupitia msimu mgumu wa kupanda na kusuka.

Ceasiaa ilimaliza nafasi ya 10 kati ya timu 12 kwenye msimamo wa ligi ikikusanya pointi 24, msimu a 2024/25 timu hiyo ilimaliza nafasi ya nne na kukata tiketi ya kucheza mashindano ya ngao ya jamii

Kocha wa timu hiyo, Ezekiel Chobanka, amesema uongozi wa klabu umejifunza kutokana na makosa ya msimu uliopita, ambapo walikosa mwendelezo wa matokeo kutokana na mapungufu yaliyokuwapo kwenye usajili.

CEA 01

Chobanka amesema baadhi ya wachezaji waliosajiliwa walishindwa kucheza kutokana na changamoto ya vibali hali iliyowalazimu kupambana hadi hatua za mwisho kuhakikisha wanabaki kwenye ligi.

“Tulijifunza mengi msimu uliopita. Tulikuwa na changamoto kwenye eneo la usajili na hilo lilituathiri kwa kiasi kikubwa safari hii tumeanza maandalizi mapema ili tusirudie makosa yale,” amesema Chobanka.

CEA 02

Kocha huyo amesema benchi la ufundi tayari limebaini maeneo yanayohitaji kuongezewa nguvu, likiwemo safu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji.

Ameongeza kuwa lengo lao siyo tu kubaki kwenye ligi, bali kujenga timu yenye ushindani itakayoweza kupambana na vigogo wa soka la wanawake.

“Tunataka kikosi kitakachoshindana katika kila mechi hatutaki tena kuingia kwenye presha ya kupambana na kushuka daraja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *