• Familia moja ya Kasarani inatafuta majibu baada ya Margaret Wambui, mwenye umri wa miaka 21, kudaiwa kuanguka kutoka ghorofa ya 22 ya Alura Apartments eneo la Upper Hill, Nairobi
  • Margaret, aliyekuwa mwanafunzi wa mafunzo kazini (intern) katika hoteli, anaripotiwa kupanda hadi kwenye paa la jengo kupiga picha kabla ya mwili wake kupatikana katika jengo jirani
  • Mama yake mwenye majonzi alisema Margaret aliondoka nyumbani kuelekea kwenye mafunzo yake kazini lakini hakuwahi kufika mahali pa kazi, na amekanusha madai kuhusu jinsi alivyoanguka

Familia moja ya Nairobi iliyo katika majonzi inataka majibu baada ya binti yao mwenye umri wa miaka 21, Margaret Wambui, kufariki dunia katika mazingira ya kutatanisha usiku wa Jumamosi, akidaiwa kuanguka kutoka ghorofa ya 22 ya Alura Apartments huko Upper Hill.

Familia ya Margaret Wambui inatafuta majibu baada ya kisura huyo kudondoka ghorofani kwa njia ya kutatanisha
Inasemekana Maragret Wambui alienda kupiga picha alipoanguka kutoka kwenye jengo hilo na kufariki. Picha: Citizen TV.
Source: Youtube

Margaret, ambaye alikuwa akifanya mafunzo kazini katika hoteli iliyoko eneo hilo, aliondoka nyumbani kwao Kasarani saa moja jioni (7:00 pm) kuelekea kazini kwa zamu yake.

Hata hivyo, hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa aliwahi kufika mahali pake pa kazi jioni hiyo.

Pia soma

Magazeti ya Kenya: Jinsi mashine ya kampeni ya Gachagua iIlivyoleta ushindi mkubwa wa 85% Ol Kalou

Kinachojulikana ni kwamba aliingia katika Alura Apartments majira ya saa nne usiku (10:00 pm).

Nini kilitokea Alura Apartments, Upper Hill?

Mashahidi wanasema Margaret alipitia mapokezi ya jengo hilo kabla ya kuelekea kwenye paa lililo kwenye ghorofa ya 22, akidaiwa kwenda kupiga picha.

Inadaiwa kuwa mlinzi aliyekuwa zamu alimwona akiwa kwenye paa hilo lakini aliondoka kwa muda mfupi kwenda chooni.

Aliporudi, Margaret hakuwepo tena.

Mwili wake haukupatikana kwenye paa bali katika jengo jirani.

Mkoba wake, uliokuwa umeachwa kwenye paa, ulikuwa na simu yake ya mkononi, sare ya kazi na vitu vingine binafsi.

Tukio hilo liliwafanya wanafamilia kufika Upper Hill saa chache baada ya kupokea simu ya kuhuzunisha kutoka kwa mmoja wa marafiki wa Margaret.

Walipokusanyika nje ya jengo hilo, walijaribu kuelewa mlolongo wa matukio yaliyopelekea kupoteza maisha kwa binti yao.

Subscribe to watch new videos

Familia ya Margaret yazungumza baada ya kuanguka kwake na kufariki

Mama wa Margaret, Wangari Gathogo, alisema alipokea simu ya kuhuzunisha kutoka kwa rafiki wa binti yake.

Rafiki huyo alimweleza kuwa alipompigia Margaret simu, mtu asiyemfahamu ndiye aliyeipokea na kumwomba awasaidie kuwapata wanafamilia ili wafike katika ofisi za DCI Kilimani.

Pia soma

Mwanaume wa Kakamega aliyefungwa jela miaka 20 baada ya kumtuma bintiye jirani dukani afungua roho

“Hakuwa na msongo wowote wa mawazo. Alikuwa akija nyumbani, anapumzika, halafu anaenda kazini siku inayofuata. Alikuwa tu sawa,” alisema mama huyo mwenye majonzi.

Kwa kuwa Margaret anaripotiwa alikuwa akitumia simu yake kupiga picha wakati alipoanguka, familia yake imekanusha vikali uwezekano kwamba alijitoa uhai.

Kupatikana kwa mkoba wake pamoja na mali zake kwenye paa la jengo kumeongeza utata kuhusu mazingira ya kifo chake.

Maafisa wa upelelezi kutoka Kituo cha Polisi cha Kilimani wameanza uchunguzi wa tukio hilo na wanatarajiwa kuchunguza picha za kamera za usalama (CCTV) zilizorekodi mienendo ya Margaret katika dakika zake za mwisho.

Uchunguzi wa maiti unatarajiwa kufanyika baadaye wiki hii, huku mwili wake ukiwa umehifadhiwa katika Hifadhi ya Maiti ya Nairobi.

Mwanamke wa Kayole aanguka kutoka ghorofa ya tano baada ya mzozo na mpenzi wake

Hapo awali, TUKO.co.ke pia iliangazia tukio la kusikitisha lililomhusisha Bellacah Wambui Kamau, mwanamke mwenye umri wa miaka 19, aliyeanguka kutoka ghorofa ya tano ya jengo la makazi huko Kayole, Nairobi, kufuatia mzozo na mpenzi wake.

Mwanamke huyo alikuwa amerudi nyumbani akiwa na matumaini makubwa ya kufanya picha za ujauzito, lakini badala yake alikumbana na taarifa ya kusikitisha iliyosababisha kifo chake cha ghafla.

Pia soma

Magazeti ya Kenya, Julai 15: Kundi la Edwin Sifuna latikisa serikali na muungano wa upinzani

Baada ya tukio hilo la kuhuzunisha, familia yake inaendelea kutafuta haki huku ikikabiliana na maumivu ya kumpoteza binti yao, ambaye maisha yake yalikatizwa ghafla katika wakati wa taharuki.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *