Leo ni Jumanne tarehe 6 Safar 1448 Hijria inayosadifiana na tarehe 21 Julai 2026

Katika siku kama ya leo miaka 814 iliyopita alizaliwa mwanafalsafa, mnajimu na tabibu mashuhuri wa Kiislamu Qutbuddin Mahmoud Shirazi katika mji wa Shiraz nchini Iran.

Alianza kujifunza tiba akiwa bado mdogo na alianza kutibu wagonjwa katika moja ya hospitali za Shiraz baada ya kufariki dunia baba yake. Katika kipindi cha miaka kumi ya kazi ya utabibu, Qutbuddin Shirazi alitalii vitabu mbalimbali vya tabibu mwingine wa Kiislamu Bin Sina na vitabu vingine vya tiba na falfasa.

Baada ya kuasisiwa kituo cha utafiti wa elimu ya nujumu katika eneo la Maraghe kaskazini magharibi mwa Iran, Qutbuddin Shirazi aliishi kipindi kirefu na mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu Khaja Nasiruddin Tusi na kupata elimu ya nujumu.

Katika kipindi chote cha umri wake, tabibu huyo wa Kiislamu alitembelea miji na nchi mbalimbali na kukutana na wasomi na maulamaa wa maeneo hayo. Ameandika vitabu vingi kikiwemo kile cha Jaamiul Usul.Alifariki dunia mwaka 710 Hijria. ***

Siku kama ya leo miaka 148 iliyopita John Boyd Dunlop raia wa Uingereza, alikuwa mvumbuzi wa kwanza wa gurudumu.

Dunlop alifikia hatua ya kuvumbua gurudumu la magari baada ya utafiti wa miaka kadhaa. Alifariki dunia 1921.   ***

Katika siku kama ya leo miaka 128 iliyopita, yaani sawa na tarehe 21 Julai mwaka 1899, alizaliwa mwandishi mtajika wa Kimarekani kwa jina la Ernest Hemingway.

Kwa muda fulani Hemingway alikuwa mwandishi huko Uingereza na Ufaransa. Hemingway alianzisha mbinu ya kuandika riwaya na tungo fupi fupi na alikuwa akitumia lugha nyepesi na inayoeleweka kwa wepesi.

Mwaka 1954 mwandishi Ernest Hemingway alitunukukiwa tuzo ya Nobel katika medani ya fasihi. Hemingway alipendelea sana kuwinda na alitumia muda mwingi katika shughuki hiyo. Alifariki dunia tarehe pili Julai 1961 baada ya kujipiga risasi na bunduki yake mwenyewe ya kuwindia, wakati akiisafisha. Hivyo, mkasa wa kifo cha baba yake ukawa umejirudia kwake baada ya kupita miaka 23.

Miongoni mwa vitabu maarufu vya Hemingway ni pamoja na kitabu cha “The Old Man and The Sea”, “A Farewell to Arms” na “For Whom the Bell Tolls”. ***

Katika siku kama ya leo miaka 72 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 21 Julai 1954 ulitiwa saini mkataba wa kuacha vita kati ya Ufaransa na Vietnam na kukomesha ukoloni wa Ufaransa huko India na China mwishoni mwa mkutano wa Geneva.

Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya kuanguka ngome imara ya Wafaransa iliyojulikana kwa jina la Dien Bien Phu nchini Vietnam Mei mwaka 1954. Makubaliano ya mkutano wa kimataifa wa Geneva, yalihudhuriwa na wawakilishi wa ngazi za juu kutoka Ufaransa, Marekani, Uingereza, China, Vietnam na Urusi ya zamani.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, vikosi vya kigeni vilipaswa kuondoka Vietnam, lakini Marekani kinyume na makubaliano ya Geneva, ikaamua kutuma majeshi katika eneo hilo kwa lengo la kuzuia kuungana maeneo mawili ya Vietnam ya kaskazini na ya kusini.  ***

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *