
Watu zaidi ya 40 wameripotiwa kutekwa nyara kaskazini mashariki mwa Nigeria wikendi iliopita, hii ni kwa mujibu wa mmoja wa manusura na serikali ya mtaa katika jimbo la Zamfara.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na vyanzo hivyo, watu wenye silaha walivamia vijiji 11 katika misururu ya uvamizi kati ya Ijumaa na Jumapili wiki iliopita, uvamizi unaotajwa kuongzwa na kiongozi wa Kundi moja la majambazi anayefahamika kama Kachalla Sa’idu.
Tukio hili la hivi punde linajiri baada ya mwezi Mei mwaka huu, zaidi ya wanafunzi 40 na Walimu kutekwa nyara na wanajihadi katika jimbo la Oyo, kabla yao kuokolewa katika oparesheni ya jeshi mapema mwezi huu.
Matukio ya utekaji nyara yameendelea kutumiwa na makundi yenye silaha kama njia ya kujipatia kipato, wakiwemo wanajihadi kaskazini mashariki na magenge ya majambazo wanaoendeleza shughuli zao kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.