
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema, bara la Afrika sasa linaongoza kwa idadi ya watu wanaokabiliwa na baa la njaa duniani. Bara la Afrika sasa limepita lile la Asia ambalo limekuwa likiongoza kwa muda mrefu.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kitengo cha chakula katika shirika la chakula na kilimo duniani ( FAO ) , David Laborde, makali ya njaa yamehamia Afrika kutoka Asia , licha ya juhudi ambazo zimekuwepo za kupunguza njaa duniani, David anasema juhudi hizo hazijakuwa na usawa.
David ameongeza kuwa China imefaulu kudhibiti makali ya njaa nchini humo kwa kipindi cha miaka 25 iliyopita, na kwa sasa India pia inajitahidi kuzuia raia wake kufariki kutokana na njaa.
Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa pia imekadiria kwamba watu zaidi ya Milioni 309 hapa Afrika waliathirika na njaa mwaka uliopita, bara la Asia likifuata ambapo watu Milioni 292 pia waliathirika.
Kwa ujumla kiwango cha njaa kilipungua kwa asilimia 8.6 mwaka 2022, ikilinganishwa na asilimia 7.8 mwaka 2025.
Mizozo kama vita vinavyoendelea nchini Sudan na mashariki mwa DRC , imetajwa kuchochea Afrika kutumbukia kwenye wimbi hili la njaa.