Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia Maria Joseph (40), mkazi wa Chang’ombe, kwa tuhuma za kuwafanyia ukatili watoto wawili, Jacob Lucas (6) na Aisha Abdul (mwaka mmoja na miezi saba).

Kwa mujibu wa Polisi, Jacob anadaiwa kupigwa kwa mwiko na kujeruhiwa, huku Aisha akidaiwa kuchomwa moto kwa kijiko kilichopashwa moto na kufungiwa ndani ya chumba. Watoto hao wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *