Serikali ya Zanzibar imetangaza ongezeko la nauli za usafiri wa umma litakaloanza kutumika Agosti Mosi mwaka huu, kufuatia mapitio yaliyofanywa kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta pamoja na maombi ya muda mrefu kutoka kwa watoa huduma za usafiri.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Khalid Salum Mohamed, amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya tathmini iliyozingatia hali halisi ya kiuchumi na gharama za uendeshaji wa usafiri.
Ameeleza kuwa kwa safari zenye umbali wa kilomita moja hadi 12, nauli imeongezeka kutoka shilingi 500 hadi shilingi 700, huku wanafunzi wakiendelea kulipa nusu ya nauli hiyo.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)