Msemo wa Waswahili unaosema “mtafutaji hachoki, na akichoka jua kapata” unaakisi safari ya mafanikio ya John Dastan Tambala, kijana aliyeanza maisha kwa kuuza samaki katika Soko Kuu la Iringa kabla ya kukutana na changamoto zilizomfanya kuhamia Dodoma na kujikita katika biashara ya mitumba.

Mwaka 2016 ulikuwa mwanzo wa mabadiliko makubwa katika maisha yake baada ya serikali kuhamia Dodoma, hatua iliyompa wazo la kuanzisha kampuni ya huduma za usafi wa ofisi akiwa na vijana 12.

Leo hii, John ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya usafi ya JODATA, ambayo imepanuka na kutoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini huku ikiwezesha ajira kwa zaidi ya watu 800.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *