Miche 5,000 ya miti imetolewa kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi wa mazingira ya Mlima Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zinazotishia ikolojia ya mlima huo.

Miche hiyo imetolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) kupitia kampeni ya GGM Kili Challenge na kukabidhiwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti uliofanyika wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Akizindua kampeni hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Hassan Omar Bomboko, ameipongeza GGML kwa mchango huo akisema unaunga mkono mkakati wa wilaya wa kupanda miti milioni 2.5 ili kuimarisha uhifadhi wa Mlima Kilimanjaro na mazingira yanayouzunguka.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Nessa, Deborah Nyakisinda, amesema mchango huo utaongeza kasi ya utekelezaji wa lengo la kupanda miti milioni mbili kila mwaka kuzunguka Mlima Kilimanjaro.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Ashraf Suryaningrat, amesema kampuni hiyo itaendelea kushiriki katika miradi ya uhifadhi wa mazingira sambamba na shughuli zake za uchimbaji, akieleza kuwa maendeleo endelevu hayawezi kupatikana bila kulinda rasilimali za asili.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *