Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) na Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tanga (TNCC) wamepinga uamuzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wa kuigeuza Stendi Kuu ya Mabasi Kange kuwa maegesho ya malori, wakitaka utekelezaji wa makubaliano ya kuboresha stendi hiyo ili iendelee kutumika kikamilifu.

Wakizungumza na waandishi wa habari, wamiliki wa mabasi wamesema wameshtushwa na kauli ya uongozi wa Jiji la Tanga ya kutaka kusitisha matumizi ya stendi hiyo, wakisisitiza kuwa wanataka Kange itumike kama ilivyokusudiwa badala ya kubadilishwa matumizi.

✍ Mariam Shedafa
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *