Wakazi wa Chanika halmashauri ya Dar es Salaam wamehimizwa kushiriki mazoezi ya kulinda afya na kujenga uhusiano mzuri miongoni mwa wanajamii.��

Akizungumza kuhusu mbio maalumu za mazoezi ‘Jogging’ zilizoandaliwa kufanyika Jumamosi ya Julai 25, 2026 kwa uratibu wa Chuo Cha Ufundi Stadi cha ‘Future World’, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Zogowali kilipo chuo hicho, Rajabu Rajabu amesema ni vyema wananchi kushiriki ‘jogging’ hilo kwa manufaa ya kijamii hususani kujenga jamii inayotambuana, yenye afya bora sambamba na kunufaika na fursa zinazotolewa na taasisi zinazofanya shughuli zake katika eneo hilo ikiwemo chuo hicho.

��Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Future World Institute, Robert Mkolla amesema ‘Jogging’ hiyo itakuwa endelevu.

��Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *