
Idadi ya visa vya Ebola vilivyothibitishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongezeka hadi 3,075, ikiwa ni pamoja na vifo 1,354, kulingana na data za serikali siku ya Jumamosi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mamlaka ya afya ya DRC imesema mlipuko huo sasa umerekodi visa 3,075 vilivyothibitishwa, ikiwa ni pamoja na vifo 1,354 na watu 556 waliopona ugonjwa huo, huku wagonjwa 755 wakisalia hospitalini au kuwekwa karantini.
Mlipuko huo unaathiri mikoa mitano, ambayo ni Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Haut-Uele na Tshopo.
Siku ya Ijumaa Waziri Mkuu Judith Suminwa Tuluka alisema kwamba watafiti wanafanya kazi katika kutengeneza dawa na chanjo dhidi ya virusi vya Ebola Bundibugyo, aina inayosababisha mlipuko wa sasa nchini DRC.
Akielezea matumaini kwamba chanjo na dawa zanaweza kupatikana “ndani ya miezi miwili hadi minne,” alibainisha kwamba serikali inafadhili utafiti huo, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu maendeleo au utaratibu uliokusudiwa wa kutoa idhini.
Kwa sasa hakuna chanjo iliyoidhinishwa au dawa iliyoidhinishwa mahususi kwa virusi vya Ebola Bundibugyo. Chanjo na dawa kadhaa ya majaribio zinafanyiwa majaribio ya kliniki.
Siku ya Ijumaa Chuo Kikuu cha Oxford kilitangaza kwamba mtu wa kwanza aliyejitolea alichanjwa katika jaribio la kwanza la kimatibabu duniani la chanjo, inayojulikana kama ChAdOx1 BDBV, iliyoundwa kulinda dhidi ya virusi vya Ebola Bundibugyo.