
RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi a ametoa maagizo kwa Shirika la Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kuvikabidhi viwanja vya mpira wa miguu kwa wahusika lengo likiwa ni kuvitumia kuendeleza vipaji vya vijana.
Kauli hiyo aliitoa Julai 23, 2026 katika uzinduzi wa usafiri wa umma kwa kutumia mabasi ya umeme uliofanyika kituo cha mabasi Malindi kisiwani Unguja.
Dk Mwinyi aliipongeza ZSSF kwa utekelezaji wa agizo la ujenzi wa kiwanja cha mpira wa miguu katika eneo hilo ambalo litawasaidia katika mahitaji yao.
“Nawataka viwanja hivi vya mpira kukabidhi kwa wahusika ili vijana waweze kuvitumia na kuendeleza vipaji vyao kisiwani hapa,” amesema.
Dk Mwinyi amesema awali timu ya Malindi ilikuwa na upinzani mkubwa kisiwani hapa kabla ya kushuka daraja msimu wa 2025-2026, hivyo, baada ya kukamilika kwa uwanja wa Matumbaku watakabidhiwa rasmi ili waweze kucheza mechi zao.