
KOCHA Mkuu wa Mafunzo, Haji Salum Haji amesema hadi sasa timu hiyo imeshasajili wachezaji wapya sita huku ikitafuta wengine watakaongeza nguvu kikosi hapo.
Kocha huyo ameliambia Mwanaspoti kutokana na usajili huo watu wategemee kuiona mafunzo yenye ushindani zaidi na sio vinginevyo.
Amesema timu hiyo imeboresha zaidi katika eneo la ushambuliaji kwa kumsajili James Mlange kutoka Fufuni kwani eneo hilo lilikuwa dhaifu msimu uliopita na wanahitaji kuongeza mmoja.
Pia, amesema timu hiyo imefanya maboresho katika eneo la kipa, pia viungo wanne.
“Msimu unaokuja mashabiki na wadau wategemee ushindani na sio kingine, msimu uliopita timu haikuwa mbovu, badala yake kuna maeneo hayakuwa sawa lakini tumeyaboresha,” amesema kocha huyo.
Kocha Salum amesema Mafunzo ilikuwa haina mfungaji hodari, kwa maana hiyo anaamini wamepata mshambuliaji mwenye uwezo na uzoefu wa kufanya mabadiliko makubwa.