#HABARI: Mbunge Mteule wa Viti Maalum watu wenye Ulemavu Ummy Nderiananga amemtaja Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi kama kipenzi cha watu wenye ulemavu nchini, akimshukuru kwa kurejesha thamani yao na kuwajengea miundombinu mbalimbali ya kuwawezesha kupata mahitaji muhimu.

Ummy amebainisja hayo leo Jumamosi Oktoba 04, 2025 Mjini Babati kwenye Mkutano wa kampeni za Mgombea Urais huyo kwenye Viwanna vya CCM Sabasaba, akisema Dkt. Samia amewezesha pia fursa za ajira kwa walemavu kutoka 146 aliowakuta mwaka 2021 hadi kufikia waajiriwa wenye ulemavu 1214, akimshukuru pia kwa kutoa kipaumbele kikubwa kwa watu wenye ulemavu katika ujio wa Bima ya afya kwa wote aliyoahidi kuanza kuitekeleza kwa majaribio ndani ya siku zake mia moja za awali madarakani.

Ummy pia amemshukuru Dkt. Samia kwa kutenga Bilioni nane zilizojenga vyuo maalumu kwa ajili ya walemavu katika Mikoa ya Kigoma, Songwe, Ruvuma na Mwanza, pamoja na shile za mjumuisho za Jendele na Pemba Pujini Visiwani Zanzibar, sambamba na ukarabati wa shule na vyuo chakavu.

Mbunge huyo mteule ameeleza pia namna ambavyo takribani Milioni 960 zilivyojenga mabweni kwaajili ya watu wenye ulemavu ikiwemo bweni lililojengwa Mkoani Manyara kwenye shule ya Endakoti, akieleza pia kuhusu mikopo kwa watu wenye ulemavu ya takribani shilingi Bilioni 45.1, ujenzi wa bweni la Viziwi Songambele na kusema kwamba hata kuulizwa kwenye zoezi la Sensa za watu na makazi ya mwaka 2022 kuhusu mahitaji yao wenye ulemavu ni kuonesha utu na kujali kwa Dkt. Samia kwa kundi hilo la watu wenye ulemavu.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *