Katika ujumbe kupitia mtandao wa Telegram, gavana wa Sumy Oleh Hryhorov, amesema wafanyakazi wa shirika la reli na abiria waliokuwa kwenye treni walijeruhiwa katika mji wa Shostka.

Ameongeza kuwa idadi ya waathiriwa inaweza kuongezeka huku juhudi za uokoaji zikiendelezwa.

Hryhorov alichapisha ujumbe huo na picha inayoonyesha kuungua kwa behewa moja la treni lakini haikubainisha aina ya silaha iliyotumika.

Zelensky asema shsambulio ni la kigaidi

Hata hivyo, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelaani kile alichokitaja kuwa shambulizi la droni dhidi ya kituo hicho.

Katika chapisho kwenye mitandao ya kijamii, Zelensky amesema lazima Urusi ilifahamu kwamba inawalenga raia na kwamba huo ni ugaidi usiopaswa kupuuzwa na ulimwengu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *