#HABARI: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Mgombea Mwenza nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, kimeendelea na kampeni zake mkoani Tabora, kunadi sera na kutoa ahadi mbalimbali kwa wananchi wa mkoa huo unaosifika kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kilimo.

Akiwa wilayani Nzega, akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu 2025, Dkt. Nchimbi, pamoja na ahadi zingine amesema chama hicho kikipata ridhaa ya kuongoza nchi kitaendelea kuboresha utoaji wa mbegu na mbolea za ruzuku pamoja na kuendelea kushirikiana na bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko (CPB) ili kuimarisha soko la mazao kwa wakulima wilayani humo.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *