
Ripoti mpya ya uchunguzi iliyotolewa inaonyesha kuwa shirika la ujasusi la utawala wa kizayuni wa Israel, Mossad ilihusika katika kutekwa nyara na kuuawa Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Aldo Moro mwaka 1978, na hivyo kudhihirisha ushawishi mkubwa iliokuwa nao Israel wakati katika uga wa siasa za Italia, ikiwa ni pamoja na kufuatia uhusiano wa Moro na makundi ya Muqawama ya Palestina.
Mwanahabari mkongwe wa Italia wa ripoti za upelelezi Erik Salerno, ambaye alitumia muda wa zaidi ya miongo mitatu kufuatilia habari za wanasiasa wakuu wa Italia, ameeleza kwa kina katika kitabu chake kiitwacho “Mossad’s Base in Italy” jinsi Italia ilivyobadilishwa kuwa “manowari ya kubebea ndege” ya kimkakati iliyokuwa ikiendeshwa kwa pamoja na Marekani na Israel.
Salerno amechunguza pia namna Israel ilivyohusika kwa siri katika utekaji nyara na mauaji ya Aldo Moro, shakhsia mashuhuri katika siasa za Italia na mwanachama mkuu wa Christian Democratic Party.
Moro, aliyetekwa nyara Machi 16, 1978 mchana kweupe na kundi la mrengo wa kushoto lenye misimamo mikali la Red Brigades, aliuawa baada ya kushikiliwa kwa siku 55. Tukio hilo lilishtua taifa la Itali na kutoa taswira mbaya katika zama za dhoruba zilizojulikana kama “Miaka ya Uongozi” ya Italia, iliyokuwa imegubikwa na njama za kisiasa na machafuko ya utumiaji nguvu.
Wakati Salerno amesita kuishutumu moja kwa moja Mossad kwa kupanga mauaji ya Moro, anaamini kuwa shirika hilo la ujasusi la Israel lilikuwa na nafasi muhimu sana katika kushadidisha mivutano ndani ya Italia, hata kwa kuunga mkono makundi yenye misimamo mikali kama vile Red Brigades kwa ajili ya kudumisha maslahi ya kijiopolitiki ya Magharibi.
Ufichuzi huo umefanywa sambamba na maandamano makubwa na migomo ya hivi karibuni iliyofanyika nchini kote Italia kuunga mkono Ghaza na kuulaani utawala wa kizayuni wa Israel kwa kuendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo…/