#HABARI: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amesema uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan umefanikiwa kuliunganisha Taifa na kuondoa dhana za udini na ukabila, jambo ambalo limeleta mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Hayo yamesemwa na Mgombea Ubunge wa Arusha Mjini kupitia Chana cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda leo Jumatatu Oktoba 6, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya ya Nyamagana, ambapo amesema Dk Samia ni zawadi kutoka kwa Mungu.

“Mimi kupewa nafasi ya kugombea ubunge Arusha ni dalili tosha ya kuwa Tanzania hamna ukabila,” amesema Makonda ambaye yupo Mwanza kushiriki mikutano ya kampeni wa Mgombea Urais wa CCM, Dk Samia Suluhu Hassan kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *