
Oktoba 7, 2023, ni siku ambayo maana yake na athari zake zinatengeneza msingi wa namna matukio ya miaka miwili iliyopita yalivyokuwa, na namna gani matukio hayo yanavyoshawishi yanayoendelea sasa.
Tukio hilo bado ni tata, kuna maswali mengi, na ukweli ambao bado haujathibitishwa:
Mashambulizi hayo yakionekana kama tukio la mapambano ya Palestina, kwa Israel kushindwa kuheshimu matokeo ya ushindi wa Hamas katika uchaguzi 2006 uliokuwa na waangalizi wa kimataifa?
Au mashambulizi hayo ni majibu ya kuishi katika mazingira ya udhalimu chini ya sera za ubaguzi za kukandamizwa?
Au Okotoba 7 inakumbukwa kama mashambulizi yaliyoyotokea bila kuchokozwa na kudhihirisha “ukatili wa Hamas” na hasa watu wote wa Palestina wa Gaza, kama alivyotangaza Rais wa Israel, Isaac Herzog?
Au Israel ilionywa na kuruhusu mashambulizi hayo kutokea ili kutimiza mpango wa kizayuni wa ‘Israel Kubwa’ kwa kupanua maeneo ya Israel hadi katika maeneo ya Palestina ya Gaza, na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, na Jerusaleme Mashariki, na katika mchakato huo kumaliza kabisa ndoto za kuwepo kwa taifa la Palestina?
Au, kwa uwazi kabisa, namna Israel ilivyojibu mashambulizi ya Oktoba 7 ilikuwa ni mpango wa mauaji ya halaiki, ambayo yalidhihirisha kuhusika kwa nchi zenye demokrasia huru za bara Ulaya na Marekani Kaskazini na udhaifu wa wa sheria ya Kimataifa na Umoja wa Mataifa kuhusu kutekeleza sheria na uwajibikaji kwa wanaofanya makosa?
Badala ya taharuki kati ya wale wanaounga mkono na wale wanaopinga Israel, watu wanaangazia zaidi matokeo ya kidiplomasia ambayo yatasaidia kusitishwa kwa mapigano, kubadilishana wafungwa, na uhakika wa kutokuwajibisha waliofanya makosa kutoka pande zote mbili.
Hatua I: Miezi baada ya Oktoba 7 – Israel iko kwenye ati ati
Licha ya viongozi wa Israel, ikiwemo Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na waziri wa zamani wa Ulinzi Yoav Gallant, kutumia lugha ya mauaji ya halaiki katika majibu yao ya awali kwa mashambulizi, neno ‘mauaji ya halaiki’ ilikuwa ni mwiko kueleza hatua za Israel.