Tanzania inatarajia kuongeza uzalishaji wa madini ya kinywe barani Afrika, kufuatia uzinduzi wa ujenzi wa mgodi wa madini hayo katika eneo la Mahenge, wilayani Ulanga mkoani Morogoro.
Mradi huo unatarajiwa kuongeza uzalishaji na kuiwezesha Tanzania kupanda kutoka nafasi ya tatu iliyo nayo kwa sasa katika bara la Afrika.
Mradi huo wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 300 unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na wawekezaji wa kampuni ya FARU Graphite.
Unatarajiwa kutoa fursa za ajira, kuimarisha miundombinu, na kuchochea ukuaji wa uchumi katika eneo hilo na taifa kwa ujumla.
Akizindua rasmi mradi huo, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, alisema mgodi wa Mahenge unaleta mwanga mpya katika sekta ya madini, ukiisaidia Tanzania kuimarisha nafasi yake kama mzalishaji muhimu wa madini ya kinywe duniani, sambamba na kuchangia maendeleo ya wananchi wa Ulanga na Morogoro.
✍️ Theresia Mwanga
#AzamTVUpdates