Kampeni nchini Cameroon, zinatarajiwa kutamatishwa kuelekea uchaguzi mkuu, uliopangwa kufanyika siku ya Jumapili, ambapo rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 92, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 43, anatarajiwa kuendelea kusalia madarakani.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kipindi cha kampeni, cha wiki mbili, kinafikia mwisho, siku mbili kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.

Katika kipindi hiki cha kampeni wagombea wawili wa upinzani wamejiondoa na kumwacha rais Biya, kupambana na wapinzani wake 12.

Mwanasiasa mashuhuri wa upinzani Maurice Kamto, aliyezuiwa kuwania urais, amewataka wafuasi wake kufanya maamuzi yao na kumchagua kiongozi wanayemtaka.

Wapiga kura Milioni nane, wamejiandikisha kwenye daftari la wapiga kura, kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi, wengi wao wakiwa vijana, wanaotarajiwa kupiga kura kwa mara ya kwanza.

Siku ya Jumatatu, rais Biya alionekana hadharani na kuhudhuria mkutano wake wa kwanza wa kampeni na kutoa hotuba ya dakika 25, alitoa ahadi mbalimbali, baada ya kurejea nchini  humo akitokea barani Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *