Dar es Salaam. Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Abdul Sykes maarufu kama Dully Sykes, amethibitisha wazi Alikiba ndiye mfalme wa muziki huo, na si mtu mwingine.

Akizungumza baada ya kuulizwa kama yeye ndiye King wa Bongo Fleva, Dully Sykes alionekana kushangazwa na swali hilo huku akitabasamu.

DUL 01

“Hapana, mimi sio Mfalme wa Bongo Fleva. Mimi ni muasisi wa Bongo Fleva. Mfalme anajulikana, Watanzania wote wanajua King ni Ali Kiba,” amesema Dully Sykes.

DUL 02

Kwa miaka mingi, Dully Sykes amehesabika miongoni mwa waanzilishi wa muziki wa Bongo Fleva, huku akitambulika kwa mchango wake mkubwa katika kukuza tasnia hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *