Dar es Salaam. Dansa anayetikisa kupitia wimbo wa Mbosso Khan “Aviola”, Queen Fraison, amefunguka kuhusu kazi yake ya unenguaji ambayo kwa sasa ndiyo inampa zaidi kipato.

Queen Fraison amesema, hapendi kucheza hadharani au kujidhalilisha, lakini hana budi kuendelea nayo kwani ndiyo kazi inayomuweka mjini.

“Sipendi kucheza hadharani au kujidhalilisha, mimi nina familia na nina wazazi kama watu wengine, lakini sina jinsi kwa sababu hii ni kazi inayolipa na siwezi kuiacha, hata familia yangu pia inalijua hilo,” amesema.

MBOS 01

Fraison ameeleza kuwa wengi hawajui umaarufu alioupata umetokana na sanaa ya kucheza, na kwa sasa amekuwa akipata mialiko mbalimbali ya maonyesho kupitia kipaji chake hicho.

“Sipo kwenye mambo mengine au tabia tofauti, nacheza, nafanya kazi, namaliza, maisha yanaendelea kwa kuwa nina familia na wazazi wanaonitazama,” ameongeza.

Amefafanua kwamba kazi yake inapaswa pia kupewa heshima sawa na sanaa nyingine, ikiwemo muziki, uigizaji, au hata kazi ya ualimu.

“Ifike kipindi mashabiki waheshimu kazi yetu, ni kazi kama nyingine yoyote mtu anavyoimba, anavyoigiza au mwanamitindo anavyofanya kazi yake,” amesema Fraison.

MBOS 02

Kwa sasa Queen Fraison anatajwa kuwa miongoni mwa wacheza shoo wanaofanya vizuri na kuvutia mashabiki kutokana na umahiri wake jukwaani.

Umaarufu wake uliibuka ghafla baada ya kuonekana akicheza wimbo wa Aviola wa kwake Mbosso Khan uliotoka Juni 13, 2025 unaopatikana kwenye albamu yake iitwayo Room Number 3 ikiwa ni nyimbo namba sita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *