#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Manyoni, Singida, imemhukumu Juma Zakale Nyenze (68), mkulima na mkazi wa Kitongoji cha Chiwondo,…#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Manyoni, Singida, imemhukumu Juma Zakale Nyenze (68), mkulima na mkazi wa Kitongoji cha Chiwondo,…

#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Manyoni, Singida, imemhukumu Juma Zakale Nyenze (68), mkulima na mkazi wa Kitongoji cha Chiwondo, Kijiji cha Sukamahela, kwenda jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 10.

Mshitakiwa alitenda kosa hilo la kikatili mnamo Agosti 22, 2025, ambapo alikamatwa na Jeshi la Polisi na kufikishwa mahakamani tarehe 29 Agosti 2025. Kutokana na ushahidi wa kutosha uliotolewa, Mahakama haikusita kutoa hukumu siku hiyo hiyo mbele ya Mh. Hakimu Itika Koroso.

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa jamii kushirikiana na vyombo vya dola kutoa taarifa mapema pale panapotokea viashiria vya ukatili dhidi ya watoto ili hatua za haraka zichukuliwe kuwalinda.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *