Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linaendelea na uchunguzi wa tukio la kupotea kwa Padri Camillus Nikata wa Jimbo Kuu la Songea, ambaye pia ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Mwanza.

Akizungumza na vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Marco Chilya, amesema Padri Nikata alifika Songea Oktoba 3, 2025 akitokea Dodoma, akiwa na mhadhiri mwenzake ambaye pia ni padre wa Jimbo la Songea. Wawili hao walifikia katika nyumba ya mapadri ya St. Shanney Oktoba 7, 2025 jioni.

Padri Nikata alionekana kwa mara ya mwisho na padri mwenzake akiwa na kibegi kidogo mkononi, akielekea stendi zamani ya mabasi Mfaranyaki, na tangu siku hiyo hajarejea alipokuwa amefikia.

Hata hivyo, uongozi wa kanisa na mapadri wenzake waliendelea na jitihada za kumtafuta katika maeneo mbalimbali waliyoamini angeweza kuwepo, lakini bila mafanikio. Ilipofika Oktoba 9, 2025 walitoa rasmi taarifa kwa Jeshi la Polisi kuhusu kutoweka kwa padre huyo.

Jeshi la Polisi bado linaendelea na uchunguzi kujua mahali alipo.

#AzamTVUpdates
✍Mawazo Mwaijengo
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *