Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imedhamiria kuendelea kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo ili kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa kitovu cha uzalishaji wa chakula katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Aidha, amesema lengo ni kuendelea kuimarisha usalama wa chakula, kupunguza utapiamlo na kuijenga Tanzania yenye wananchi wenye afya bora, nguvu kazi imara na uchumi unaojitegemea.

Majaliwa amesema hayo leo Oktoba 16, 2025 katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani ambayo kitaifa yamefanyika Uwanja wa Shule ya Sekondari Usagara, mkoani Tanga.

#AzamTVUpdates
Mhariri | @claud_jm

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *