#HABARI: Mnamo Oktoba 15, 2025 katika Mahakama ya Wilaya ya Rombo mbele ya Mhe. Innocent Nyella Hakimu Mkuu Mwandamizi, imeamriwa kesi ya jinai namba 9081/2025 ikiwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Bw. Hemrod Elias Ngunga Fundi Bomba wa ROMBOWSSA. Bw. Ngunga, alishtakiwa kwa kosa la kushawishi, kuomba na kupokea hongo chini ya vifungu vya 15 (1)(a)(b)( 2) vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya Mwaka 2022.
Mawakili wa Serikali Bi. Furahini Kibanga na Bw. Anold Mafwele, wameieleza mahakama kuwa mshtakiwa akiwa Fundi Bomba katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Rombo (ROMBOWSSA), alishawishi aliomba na kupokea hongo ya kiasi cha Tsh. 20,000/= kutoka kwa mteja, ili aweze kumrejeshea mteja mita zake zilizokuwa zimeibiwa maeneo ya Holili.
Mahakama imemkuta mshtakiwa na hatia na kumuamuru kulipa faini ya Tsh. 300,000/= au kwenda jela miaka mitatu, mshtakiwa ameshindwa kulipa faini hivyo amepelekwa rumande.
•Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania