Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Bara, Mussa Mwakitinya amekutana na makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo wajasiriamali, wafanyabiashara na maafisa usafirishaji, akiwahamasisha kumpigia kura mgombea wa urais wa chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akizungumza na vijana maafisa usafirishaji wa bodaboda, wilayani Mbogwe, mkoani Geita, Mwakitinya amesema serikali chini ya Dkt. Samia, imetoa mchango wa shilingi milioni 124 kwa ajili ya mikopo ya pikipiki wilayani humo.

Aidha, Mwakitinya amesema kuwa kupitia utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020–2025, serikali ya awamu ya sita imetengeneza ajira zaidi ya milioni nane, idadi inayozidi lengo la ajira milioni nane zilizokuwa zimepangwa kufikiwa kufikia mwaka 2025.

Mhariri @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *