Laigwanani Mkuu wa Jamii ya Kimasai, Isack Ole Kisongo Meijo, ametangaza kusogezwa mbele kwa zoezi la tohara kwa vijana wa Kimasai ili kutoa nafasi kwa zaidi ya vijana elfu mbili kushiriki kupiga kura Oktoba 29, 2025.
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla Meijo amesema jamii ya Kimasai imeamua kulinda amani na kujitokeza kwa wingi kupiga kura, huku Makalla akiwasisitizia umuhimu wa kudumisha utulivu wakati wa uchaguzi.
✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates