Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa makundi mbalimbali ya kijamii kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kijamii.
Majaliwa amesema kuwa Serikali inafanya hivyo kwa kutambua kuwa kundi la wajasiriamali ni muhimu na nguzo katika kukuza uchumi wa Taifa.
Amesema hayo leo katika mkutano wake na makundi mbalimbali ya wajasiriamali wa jijini Dar es Salaam, uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).
#AzamTVUpdates
✍ Warda John
Mhariri | @claud_jm