#HABARI: Mbunge wa viti maalum mstaafu kupitia CHADEMA, Felista Njau, amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amevunja mfumo dume kwa vitendo na kuwataka wanawake wa Mkoa wa Mara kujitokeza kwa wingi kumpigia kura katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza mjini Musoma kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Mgore Kigera, Njau amesema Dkt. Samia ameleta mageuzi makubwa ya kijamii na kiuchumi ambayo yamewapa wanawake nguvu, fursa na usawa katika maeneo mbalimbali ya maisha.

“Nimekuja kutoka Kilimanjaro kwa rafiki yangu. Niko mbele yenu, wanamusoma, kuwaomba kura tatu bomba kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mwanamke shujaa aliyeonyesha mambo makubwa,” alisema Njau huku akishangiliwa na umati wa wakazi wa Musoma Mjini.

•Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *