
Raila Odinga sasa amepumzika pamoja na babake katika kaburi la familia huko Bondo. Katika mji huu wa magharibi mwa Kenya, ambapo mazishi yake yalifanyika siku ya Jumapili, Oktoba 19, hisia zilmeongezeka.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu maalum huko Bondo, Albane Thirouard
Jeneza la Raila Odinga likiwa limefunikwa na bendera ya Kenya limepokelewa na maelfu ya wafuasi katika chuo kikuu ambako mazishi yake yalifanyika. Ibada ya mazishi iliendelea hadi mchana.
Oburu Odinga, kaka wa Waziri Mkuu wa zamani, alihuzunishwa na kifo cha “rafiki yake mkubwa.” “Mnamo mwaka 1982, kulipokuwa na jaribio la mapinduzi na ndugu yangu alikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini, nilienda kumuona katika Gereza la Kamiti,” alisimulia. “Na nilimwona, akiwa amevalia sare nyeusi ambayo kawaida huwekwa kwa wale wanaokabiliwa na adhabu ya kifo. Nililia, na akacheka, akisema hakuna jambo lolote litatokea. Raila alikuwa jasiri sana. Alipopigania haki, hakuwahi kuogopa chochote.”
Hotuba hizo pia zilichukua mkondo wa kisiasa. Wanachama kadhaa wa chama cha Raila Odinga walitoa wito wa umoja. Rais William Ruto, ambaye aliunda naye serikali ya umoja mwaka mmoja uliopita, pia alirejelea hili: “Baba aliamini vyama vya kisiasa; alijenga chama kikubwa zaidi cha kisiasa, ODM. Tutaheshimu ODM; tutawaunga mkono ili ODM iendelea kuwa na umoja.” ODM lazima ibaki imara uchaguzi wa mwaka 2027 unapokaribia, kwa sababu hivyo ndivyo tutakavyokuwa na serikali imara.”
Kiongozi huyo wa upinzani na mgombea urais ambaye alishindwa mara tano, ambaye pia alishikilia nafasi ya Waziri Mkuu alifariki siku ya Jumatano, Oktoba 15, nchini India akiwa na umri wa miaka 80. Kurejeshwa kwa mabaki yake nchini Kenya kulifuatiwa na siku tatu za hamasa kali. Watu watano walipoteza maisha wakati wa mikusanyiko ya watu jijini Nairobi.
Raila Odinga alizikwa katika kaburi la familia. Wafuasi wake kisha walifurika kwenye makaburi kutoa heshima zao za mwisho kwa mpinzani huyo wa kihistoria na wa muda mrefu.