#HABARI:Mkutano uliokuwa ukisuburiwa kufanyika kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Budapest Hungary, umesitishwa kwa muda baada ya Urusi kutupilia mbali suala la kusitisha mapigano.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio baada ya kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov.

Trump amethibitisha taarifa hiyo huku akisema hahitaji kuwa na mkutano usio na tija wala kupoteza muda.

Urusi kwa upande wake imesema maandalizi ya mkutano huo kati ya Trump na Putin yanaendelea lakini kwanza kunahitajika kukubaliana katika mambo kadhaa muhimu.

Ikulu ya Kremlin imetoa tangazo baadaye na kusisitiza kuwa masharti yake ili kufikia amani nchini Ukraine bado hayajabadilika.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *