Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Hamad Mbega, amewataka vijana wanaonufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Wilaya hiyo, kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kuanzisha na kuendeleza miradi ya kiuchumi, badala ya kuzitumia kwa anasa au matumizi yasiyo na tija.
Mbega amesema lengo la Serikali kutoa mikopo hiyo ni kuwawezesha vijana kujitegemea kiuchumi na kuchangia maendeleo ya Taifa, hivyo ni muhimu fedha hizo zikatumika kwa uadilifu na nidhamu ya kifedha.
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates