#HABARI: Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Kampuni yake Tanzu ya Uendelezaji Jotoardhi (TGDC) kuhakikisha kuwa vifaa vyote vya uhakiki wa rasilimali Jotoardhi katika mradi wa Ziwa Ngozi vinafika kwa wakati ili kazi za uhakiki ziweze kumalizika kulingana na muda uliopangwa.

Dkt. Mataragio ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake ya kukagua kazi zinazoendelea kutekelezwa katika mradi huo wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

“Huu mradi mnapaswa kuukamilisha kwa wakati kutokana na umuhimu wake nchini, tunapotekeleza miradi hii ya Jotoardhi tukumbuke kuwa tunatekeleza pia Sera ya Taifa ya Nishati ya Mwaka 2015 ambayo inasema Tanzania inapaswa izalishe umeme kwa kutumia vyanzo mchanganyiko (generation mix) ambapo jotoardhi ni mojawapo.” Amesema Dkt. Mataragio

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *