
Rais wa mpito wa Mali amewafuta kazi makamanda watatu waandamizi wa jeshi, taarifa kutoka kwa baraza la mawaziri zimeonesha siku ya Jumatano.
Rais Assimi Goita amemtimua naibu kamanda wa jeshi, mkuu wa usalama jeshini na mkuu wa majeshi ardhini, taarifa hiyo ilisema.
Shirika la AFP limearifu kuwa watatu hao walifutwa kwa “utendakazi mbaya” katika uwanja wa vita, wakimtaja afisa mmoja mwandamizi.
Tangu 2012 Mali imekuwa na matatizo ya kiusalama kutokana na mashambulizi ya magaidi wenye uhusiano na makundi ya Al Qaeda na Daesh.