Dar es Salaam. Nyota wa Bongofleva, Diamond Platnumz amesema  mke wake Zuchu ambaye pia ni msanii wake kupitia Lebo ya WCB, amekuwa kama taa kwake kutokana na uzuri alionao.

Akizungumza na Mwananchi, amesema anajiona ni mwanaume mwenye bahati kuwa na msichana mrembo kama mke wake huyo na ni mwanamke ambaye anampenda sana.

“Kwa kweli mimi mwenyewe Zuchu nikimuangalia nasikia raha sana, anakuwa kama taa kwangu na sio kwangu hata kwa watu wengine wananiambia nina kifaa cha nguvu kabisa ndio maana naringa naye na kutamba naye kila sehemu,” amesema Diamond.

Aidha, Diamond alikanusha habari za kumtumia Zuchu kumuingizia pesa kwenye lebo na sio kumpenda kimapenzi.

“Ujue habari nyingine huwa nazisoma na kucheka, sijui hata watu huwa wanawaza nini, sasa wanavyosema mimi namtumia Zuchu kuniingizia pesa, ina maana mimi siingizi pesa? Kwamba sifanyi kazi namtegemea Zuchu sasa si ndio?

“Nina vyanzo vingi vya kupatia pesa kwanini waseme namtumia mtoto wa watu? Ebu waache kusema hivyo na wamuache Zuchu wangu jamani, wasimkatishe tamaa kwenye safari yake ya muziki,” amesema Mondi.

Diamond na Zuchu walifunga ndoa Juni 2025, iliyokuwa ya kimya kimya bila hata ya wazazi wao na baadhi ya watu wao wa karibu kuhudhuria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *