#HABARI: Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso amewataka wananchi wa Jimbo la Segerea kuwa waangalifu katika kipindi hiki cha uchaguzi kwa kujiepusha na wanasiasa anaowaita matapeli wa kisiasa wasiokuwa na dira wala sera za maendeleo.
Akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Msikate Tamaa, Kata ya Vingunguti, Paresso alisema baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakijitokeza tu wakati wa uchaguzi na kutoa ahadi zisizotekelezeka bila kuwa na mipango halisi ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Alieleza kuwa, tofauti na wanasiasa hao, serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutekeleza miradi yenye tija katika Jimbo la Segerea, ikiwemo ujenzi na ukarabati wa barabara katika mitaa mbalimbali, uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwa kujenga na kukarabati madarasa katika shule za msingi na sekondari, pamoja na kuboresha kituo cha afya cha Segerea ambacho sasa kinatoa huduma bora zaidi kwa wananchi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.