#HABARI: Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Pwani, kimekanusha taarifa zinazodai kuwa chama hicho kimewataka walimu kutoshiriki katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, huku kikieleza kuwa madai hayo ni ya uongo na yamelenga kuleta taharuki pamoja na kuwagawanya walimu na Umma wa Watanzania.
CWT imesisitiza kuwa haijawahi kutoa maelekezo yoyote yanayozuia ushiriki wa walimu katika uchaguzi, na imewataka wanachama wake kupuuza taarifa hizo ambazo zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari.
Akizingumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Pwani, Hamdani Kisoma, na Katibu wake, Suzan Shesha, wamesema chama hicho kimetoa wito kwa walimu wote nchini kushiriki kikamilifu katika zoezi la upigaji kura, wakisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kutimiza haki yao ya kikatiba.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.