#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Mkoani Ruvuma, Bi.Ngollo Malenya, amesema hakuna tishio lolote la uvunjifu wa amani katika wilaya hiyo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, huku akiwahakikishia wananchi kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vimejidhatiti kuhakikisha zoezi la uchaguzi linafanyika kwa utulivu na amani.
Bi. Malenya amesema maandalizi ya uchaguzi huo yamefikia hatua nzuri huku akiwataka wananchi wote wenye sifa ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura hapo kesho Oktoba 29, 2025, na kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi wanaowafaa katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.