Kamati za ulinzi na usalama za mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba zimewahakikishia wananchi kuwa hali ya amani na utulivu itaendelea kudumishwa katika kipindi chote cha uchaguzi na hata baada ya kukamilika kwa mchakato huo.
Viongozi hao wamewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kikatiba kuwachagua viongozi wanaowataka, kisha kuendelea na shughuli zao za kila siku bila hofu yoyote.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi