Wizara ya Vita ya Marekani imeamuru wanajeshi wa Gadi ya Taifa kuunda kikosi kipya haraka kwa ajili ya kukandamiza zaidi raia wanaolalamikia uongozi mbovu wa Trump katika majimbo yote ya Marekani. Kikosi hicho kitapewa nguvu zote za kukandamiza maandamano ya wananchi ya kupigania haki zao.

Shirika la Habari la Fars limelinuku gazeti la Marekani la The Wall Street Journal likifichua kwamba, Wizara ya Vita ya nchi hiyo Pentagon imeiamuru Gadi ya Taifa katika majimbo yote ya Marekani kuunda vikosi maalumu vitakavyoitwa vikosi vya radiamali ya haraka ili kukabiliana na hali mbaya iliyoikumba Marekani hivi sasa. Vikosi hivyo vitaundwa kabla ya mwezi Januari 2026.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, lengo la kuundwa vikosi hivyo ni kujiandaa “kukabiliana na vita na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika miji mbalimbali ya Marekani.

Gazeti hilo limeendelea kufichhua kuwa, amri hiyo ilitolewa Oktoba 8, 2025 na Jenerali Ronald Barrack, Mkurugenzi Ofisi ya Jeshi la Ulinzi wa Taifa la Pentagon na inalitaka kila jimbo la Marekani kuwa na kwa uchache askari  500 waliopata mafunzo maalumu ya kukandamiza wananchi wakati wa maandamano, kukabiliana na vizuizi na wanaojua kutumia vifaa vya kupambana na ghasia na kupunguza nguvu za mapigano uwanjani.

Hatua za ukandamizaji na za kibaguzi zinazochukuliwa na Trump zimesababisha malalamiko makubwa ndani ya Marekani kiasi kwamba hata zinatishia kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Wakosoaji wa Trump na serikali yake inayowapendelea Wazungu na kudharau watu wa jamii nyinginezo huko Marekani wanasema kuwa, hatua hizo za Trump ni za kuzidisha tu fikra za kibaguzi za kujiona bora Wazungu mbele ya wananchi wengine wa Marekani.

Kwa upande wake gazeti la Washington Post limeandika kuwa, baadhi ya wakuu wa majimbo ya Marekani hawafurahishwi na uamuzi huo wa Trump wakisema kuwa unaingilia nguvu zao za kiutawala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *