Zaidi ya watu 40 kufukia sasa wamethibitishwa kufariki katika mkasa wa maporomoko ya udongo ya wiki iliopita katika eneo la bonde la ufa nchini Kenya, mpaka na nchi ya Uganda.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakati huu juhudi za uokoaji zikiendelea, baadhi ya familia zilizopoteza wapendwa wao bado zinakabiliwa na wakati mgumu kutokana na kilichotokea, wengine wakiwa wamewapoteza zaidi ya watu watatu kutoka familia moja.
Kulingana na Waziri wa usalama wa ndani wa Kenya Kipchumba Murkomen, kuna hofu ya kutokea kwa maporomoko mengine ya udongo kwenye eneo la binde la Kerio kutokana na mvua kubwa ambayo inaendelea kunyesha, raia walio katika maeneo hatari wakihamishwa.

Wanafunzi 14 ni miongoni wa Wakenya waliofariki kwenye maporomoko hayo kwenye eneo la bonde la ufa kulingana na Wizara ya elimu ya Kenya.
Kwa upande wa Uganda, Shirika la Msalaba Mwekundu limeripoti karibia watu 18 walifariki mashariki mwa nchi hiyo na kwamba mamlaka ingali inaendelea kuwatafuta watu wengine zaidi ya 20 ambao hawajulikani walipo katika wilaya za Kapchorwa, Bukwo na Kween.