
Kiongozi wa mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Leo XIV Jumapili ya leo ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano nchini Sudan na kuruhusu kufunguliwa kwa njia kupitisha misaada ya kiutu nchini humo. Kiongozi huyo ameeleza kuhuzunishwa na ripoti za ukatili wa kutisha katika mji wa Al Fashir katika jimbo la Darfur.
Papa Leo ameitolea mwito jamii ya kimataifa kuchukua hatua na maamuzi ya kusaidia juhudi za uokozi kwa watu wa Sudan. Siku ya Ijumaa, Umoja wa Mataifa ulisema kwamba mamia ya watu wameuliwana kundi la wanamgambo wa RSF katika mji wa Al Fashir ambao ulikuwa ni ngome ya mwisho ya jeshi la Sudan.
Mbali na yanayoendelea Sudan, Papa pia amegusia hali tete inayoendelea nchini Tanzania baada ya uchaguzi akizitaka pande zote kuepuka vurugu na kufuata njia ya mazungumzo.