Tume ya Umoja wa Afrika imemteua mjumbe wake mpya maalum nchini Jamhuri ya Madagaska. Naye  ni Balozi wa Djibouti, Mohamed Idris Farah.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mohamed Idris Farah ambaye alikuwa mwakilishi wa kudumu wa Djibouti katika Umoja wa Afrika, AU, misheni yake itakuwa kukuza mazungumzo kati ya vpande mbalimbali nchini Madagascar na kuunga mkono kurejea kwa utaratibu wa kikatiba, kama ilivyoainishwa katika ajenda ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kwa kusaidia kuondokana na mgogoro wa kisiasa nchini Madagascar.

Kulingana na AU, mamlaka ya Bw. Farah yanajumuisha kuimarisha ushirikiano na mamlaka za serikali, viongozi wa vijana, mashirika ya kiraia, wadau wa kikanda na mashirika, na wadau wote husika, kwa lengo la kukuza mazungumzo jumuishi, kufikia makubaliano, na kukuza uelewa wa pamoja kwa ajili ya utatuzi wa amani wa mgogoro huo na kurejesha haraka utaratibu wa kikatiba katika taifa hili.

Kama ukumbusho, maandamano yalizuka Madagascar mwishoni mwa mwezi eptemba, ambayo mwanzoni yalisababishwa na uhaba mkubwa wa umeme na maji. Baadhi ya maandamano haya yaliongezeka na kuwa vurugu na kugeuka kuwa wito wa rais kujiuzulu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *