
Watu 48 wameuawa nchini Cameroon, kufuatia maandamano ya wapinzani kupinga ushindi wa rais Paul Biya, mwenye umri wa miaka 92 kuendelea kuongoza kwa muhula wa nane.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Maandamano hayo yaliitishwa na mpinzani wake mkuu Issa Tchiroma, ambaye alidai kushinda uchaguzi huo na hata kusema, kuna baadhi ya wanajeshi wamempa ulinzi.
Ripoti za Umoja wa Mataifa zimeeleza kuwa watu hao walipoteza maisha, baada ya kupigwa risasi na maagisa wa usalama na kuwaacha wengine na majeraha mabaya.
Taarifa zaidi zinasema, watu hao waliopoteza maisha, waliuawa papo hapo kwa kupigwa risasi huku wengine, wengine wakipoteza maisha, wakipokea matibabu hospitalini.
Hata hivyo, serikali imekanusha madai ya maafisa wa usalama, kutumia nguvu kupita kiasi, huku Waziri wa usalama Paul Nji, akionya kuwa Tchiroma, atachukuliwa hatua kali kwa kuchochea fujo za baada ya uchaguzi.