Katika ujumbe wake, Guterres amesema maandalizi hayo yanahusisha kuweka mifumo ya kutoa maonyo ya mapema au tahadhari kwenye kila ufukwe, jamii na kokote kule.

Tsunami hutokea kwa nadra lakini madhara makubwa

Guterres amefafanua kuwa tsunami si matokeo ya mara kwa mara lakini pindi yanapotokea madhara yake yanaweza kuwa makubwa na hata kusababisha vifo.

“Husababisha vifo vya maelfu n ahata mamia ya maelfu ya watu. Lakini kuna mbinu za kuweka watu salama,” amesema Guterres.

Ametolea mfano janga la tsunami kwenye bahari ya Hindi mwaka 2004, janga ambalo lilisababisha dunia kuamua kuwekeza katika mifumo ya kutoa maonyo mapema.

“Miongo kadhaa baadaye, uamuzi huo umelipa,” amesema Katibu Mkuu akitolea mfano tetemeko kubwa la ardih lililokumba pwani ya Urusi mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu.

“Lilisababisha tahadhari kwa mamilioni ya watu kuanzia pwani za Japani hadi visiwa vilivyoko bahari ya Pasifiki hadi California,” amesema Katibu Mkuu.

Taswira kutoka angani ya uharibifu mkubwa wa pwani ya Indonesia, kati ya miji ya Banda Aceh na Meulaboh. Picha ilipigwa wiki moja baada ya tsunamii ya Bahari ya Hindi ya mwaka 2004.

UN Photo/Evan Schneider

Taswira kutoka angani ya uharibifu mkubwa wa pwani ya Indonesia, kati ya miji ya Banda Aceh na Meulaboh. Picha ilipigwa wiki moja baada ya tsunamii ya Bahari ya Hindi ya mwaka 2004.

Mifumo ya maonyo iimarishwe iende na wakati

Ingawa hivyo amesema madhara ya janga hilo la tsunami yanaendelea kubadilika kutokana na mabadiliko kadhaa ikiwemo yale ya tabianchi.

Kiwango cha maji ya bahari kikiongezeka, na idadi ya watu wanaoishi maeneo ya pwani ya bahari ikiongezeka, mifumo ya kutoa maonyo mapema nayo inahitaji uwekezaji zaidi na kuboreshwa,” amesema Guterres, akisema kuwa kuheshimu baharí ni kutambua nguvu yake.

Ni kwa mantiki hiyo amesema hilo ndio lengo la mpango wa Umoja wa Mataifa wa Mfumo wa Tahadhari kwa Wote ulioanzishwa kwa lengo la kuhakikisha kila mtu anafikiwa na mpango wa utoaji onyo mapema dhidi ya tsunami ifikapo mwaka 2027.

Maadhimisho ya mwaka huu ni ya 10, ambapo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilianzisha siku hii kupitia azimio namba 70/203 la mwaka 2005.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *