
Dar es Salaam. Mitandao ya kijamii imeendelea kuwa sehemu muhimu kwa wasanii wa Bongo Fleva kujenga majina yao, kutangaza kazi na kuwasiliana na mashabiki. Hata hivyo kwa siku za karibuni hali imekuwa tofauti baada ya mastaa kadhaa kujikuta wakipoteza maelfu ya wafuasi (followers) kwa muda mfupi.
Kwanza kabisa ni nguli wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ambaye licha ya kufanya vizuri na wimbo wake ‘Sasampa’, amepoteza zaidi ya 10,000 followers ndani ya kipindi cha takribani siku tano kuanzia Oktoba 30 hadi Novemba 4, 2025. Taarifa zinaonesha kuwa Novemba 5 pekee, ndani ya saa 15, akipoteza takribani wafuasi 34,000.
Mfalme huyo wa WCB hakuwa pekeyake. Mwanamuziki Zuchu, ambaye hivi karibuni ametikisa na ngoma yake ‘Amanda’, naye ameonja joto la jiwe baada ya kukadiriwa kupoteza zaidi ya 6,900 followers kati ya Oktoba 29 hadi Novemba 5, 2025.
Kwa upande wa Harmonize ambaye mara zote amekuwa gumzo mitandaoni naye amejikuta akishuka kwa zaidi ya 10,000 followers. Huku zaidi ya 5,400 wakipotea kwa siku moja tu Novemba 3, 2025.
Msanii mwingine aliyeathirika ni Rayvanny, ambaye naye ameendelea kuona idadi ikishuka siku baada ya siku. Taarifa zinaonesha kuwa ndani ya siku tano tu amepoteza zaidi ya 12,700 followers, ambapo Novemba 4 alipoteza wafuasi 5,349 huku Novemba 5, akipoteza 5,100. Lakini inaelezwa kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka kwa siku za mbeleni.
Hata hivyo, kwa upande wa Alikiba, hali haijawa mbaya kama kwa mastaa wengine, kwani amepoteza takribani wafuasi 5,800 ndani ya siku nne